Kiingereza: Greetings
Jinsi ya kutamka (Gritings)
Katika lugha yoyote mara nyingi salam ndiyo huwa kitu cha kwanza. Hivyo basi soma kwa makini somo hili la kwanza ili ujijengee uwezo wa kusalimia kwa kiingereza.
Kwa hakika katika salam za lugha ya kiingerza hakuna neno lenye maana au tafsiri ya shikamoo, ila kuna salamu zinazozingatia sana muda au wakati husika.
Hivyo asubuhi kuna salam yake, mchana kuna salam yake, hali kadhalika jioni na usiku.
Katika salam za kiingereza Neno Good tamka (Gud) tafsiri yake kwa Kiswahili ni Njema au Mwema
Neno Morning, tamka (moningi) tafsiri yake ni Asubuhi.
Neno Afternoon, tamka (aftanuni) tafsiri yake ni Mchana.
Neno Evening, tamka (ivining) tafsiri yake ni Jioni.
Neno Night, tamka (naiti) tafsiri yake usiku.
Salam za kiingereza huanza kutamkwa na mtu yeyote kati ya mukubwa na mdogo, hii ni tofauti na shikamoo katika Kiswahili ambayo lazima ianze kutamkwa na mdogo.
Salam za kiingereza huwa kama ionekanavyo hapo chini.
Good morning! (Gudi moning) – Asubuhi njema
Jibu: Good morning! (Gudi moning) – Asubuhi njema
Good afternoon! (Gudi aftanuni) – Mchana mwema
Jibu: Good afternoon! (Gudi aftanuni) – Mchana mwema
Good evening! (Gudu ivining) – Jioni njema
Jibu: Good evening! (Gudu ivining) – Jioni njema
Good evening hutumika mpaka usiku katika salam, endapo good night haitakuwa na maana au tafsiri ya salam, ila itakuwa na maana au tafsiri ya Kalale salama, au Lala salama, au Alamsiki.
Watu wengi hujichanganya kwa kutamka Good night tamka (Gudi naiti) na kudhani kuwa ni salamu ya usiku.
Salam za Good Morning, Good Afternoon na Good Evening pia zaweza kufuatiwa na salam zifuatazo:-
How are you? (Hau a yu)? - U hali gani?
Jibu laweza kuwa: -
I am fine (Ai Em faini) - Mimi ni mzima.
I am not fine (Ai En noti_faini) - Mimi siyo mzima.
I am very fine (Ai Em veri faini) - Mimi ni mzima sana.
I am not very fine (Ai Em noti_veri faini) - Mimi siyo mzima sana.
How are things? (Hau a thingsi)? - Vipi mambo?
Jibu laweza kuwa:-
Fine (Faini) - Mazuri.
Not fine (Not faini) - Siyo mazuri.
Very fine (veri faini) - Mazuri sana.
Not very fine (noti very faini) – Siyo mazuri sana
Bad (badi) – Mabaya.
Not bad (Noti badi) – Siyo mabaya.
Very bad (Veri badi) – Mabaya sana.
Not very bad (Noti veri badi) – Siyo mabaya sana.
Cool (kulu) - Poa
Not cool (Noti kulu) - Siyo poa.
Very cool (very kulu) – Poa sana.
Not very cool (Noti very kulu) - Siyo poa sana.
The things are fine (Dhe thingsi a faini) - Mambo ni mazuri.
The things are not fine (Dhe things a noti faini) - Mambo siyo mazuri.
The things are very fine (Dhe thingsi a veri faini) - Mambo ni mazuri sana.
The things are not very fine (Dhe things a noti veri faini) - Mambo siyo mazuri sana.
The things are bad (Dhe thingsi a badi) - Mambo ni mabaya.
The things are not bad (Dhe thingsi a noti badi) - Mambo siyo mabaya.
The things are very bad (Dhe thingsi a veri badi) - Mambo ni mabaya sana.
The things are not very bad (Dhe thingsi a not veri badi) - Mambo siyo mabaya sana.
The things are cool (Dhe thingsi a kulu) – Mambo poa.
The things are not cool (Dhe thingsi a noti kulu) – Mambo siyo poa.
The things are very cool (Dhe thingsi a veri kulu) – Mambo poa sana.
The things are not very cool (Dhe thingsi a noti veri kulu) – Mambo siyo poa sana.
How this Morning? (Hau dhisi moning)? - Vipi Asubuhi hii?
Jibu laweza kuwa kama ifuatavyo:-
This Morning is cool (Dhisi moning iz kulu) – Asubuhi hii ni poa.
This Morning is not cool (Dhisi moning iz noti kulu) – Asubuhi hii siyo poa.
Kwa ufupi jibu laweza kuwa moja kati ya majibu yaliyopita hapo juu.
Endapo mtu atatoa jibu lioneshalo hali au mambo yake kuwa siyo mazuri,
kwa mfano, - I am not fine. Waweza pia kumuuliza yafuatayo:-
What is your problem? (wati iz yua problem)? - Tatizo lako ni nini?
Jibu Iaweza kuwa: I am sick (Ai Em siki) - Mimi ni mgonjwa.
Au pia swali Iaweza kuwa kama ifuatavyo:-
What is wrong with you? (Wati izi rong widhi yu) - Unakabiliwa na baya lipi?
Jibu laweza kuwa kama ifuatavyo:-
My book has been stolen.
Jinsi ya kutamka - (Mai buku hazi bini stolen)
Kitabu changu kimeibwa.
Wasiliana Nasi Kupitia Mawasiliano Yetu Hapo Chini Kujua Namna Ya Kujiunga Na Maelezo Zaidi
0 Comments